Wanasayansi wanasema kuwa kufanya kazi
katika muda usio wa kawaida kikazi au katika
mazingira yaliyo ya upweke kunaweza
kuzeesha ubongo na kufanya uwezo wa
utendaji kuwa duni.
Utafiti huo umeeleza katika jarida la
Occupational and Environmental Medicine kuwa
iwapo kazi za kupokezana, mfano nyakati za
usiku zitafanywa kwa takriban miaka kumi
mfululizo zitazeesha ubongo kabla ya wakati
wake.
Wanasayansi wanasema ahueni imeonekana
kwa watu baada ya kuacha kufanya kazi hizo
lakini ilichukua miaka mitano kurejea kwenye
hali ya kawaida.
Utafiti huu unaelezwa kuwa muhimu, kwa kuwa
waathiriwa wengi kutokana na tatizo hilo
wamekuwa wakilala usingizi wa
mang'amung'amu.
Moja ya madhara yatokanayo na kufanya kazi
usiku ni kuongezeka uzito kupita kiasi
Wataalam hawa wameiambia BBC kuwa miili na
akili zimejengwa kwa kufanya kazi mchana na
kulala nyakati za usiku.
Athari mbaya ambazo zinaelezwa kutokana na
mtindo huo wa ufanyaji kazi ni madhara ya
Saratani na uzito mkubwa.
Timu ya wanasayansi kutoka chuo cha Swansea
na Toulouse wameonesha kuwa kuna madhara
ya kiakili pia.
Post a Comment