Jeshi la Burkina Faso ambalo linadhibti
nchi hiyo kufuatia kujiuzulu Blaise Compaore, Rais aliyeshikilia
madaraka ya nchi hiyo kwa muda mrefu,
limesema kuwa hatua ya kukabidhi
madaraka inawezekana kutekelezwa katika muda wa wiki mbili.
Luteni
Kanali Isaac Yacouba Zida, Kaimu Rais wa Burkina Faso amesema kuwa
hakuna sababu ya kutoweza kukabidhi madaraka kutoka utawala wa kijeshi
katika kipindi cha wiki mbili, iwapo kila mmoja ataafiki suala hilo.
Jumamosi iliyopita, jeshi la Burkina Fasoo lilimteua Luteni Kanali Zida
Naibu Kamanda wa kikosi cha ulinzi wa Rais kuongoza kipindi cha mpito.
Zida amesema kuwa Burkina Faso
itaongozwa na kikosi cha mpito katika fremu ya katiba na kusisitiza kuwa
mamlaka hiyo ya utawala ilipasa kuongozwa na kiongozi aliyechaguliwa na
makundi yote ya jamii
Post a Comment