Benki ya Dunia imesema kuwa nchi za Asia
zimeshindwa kutoa msaada wa kutosha katika mapambano ya kimataifa dhidi
ya Ebola, licha ya kuwa na wafanyakazi wa kutosha wenye ujuzi wa sekta
ya tiba. Hayo yameelezwa Jumanne hii na Jim Yong Kim, Mkuu wa Benki ya
Dunia katika mkutano na vyombo vya habari huko Seoul mji mkuu wa Korea
ya Kusini. Kim amewataka viongozi wa nchi za Asia kutuma wataalamu wa
afya huko Liberia, Guinea na Sierra Leone, ambako mlipuko wa homa ya
Ebola umeua watu karibu ya elfu tano.
Mkuu wa Benki ya Dunia ameongeza kuwa,
na hapa ninamnukuu" tunahitaji maelfu ya wafanyakazi wa huduma za afya,
na tutaendelea kuwahitajia katika kipindi cha zaidi ya miezi sita ijayo.
Mapambano dhidi ya Ebola hayajakwisha hadi kutakapokuwa hakuna kesi
yoyote katika nchi hizo tatu",mwisho wa kunukuu.
Post a Comment