Wizara ya Mambo ya Nje ya Tunisia imeyataka makundi yote ya Walibya
walioko Tunisia kuacha kujishughulisha na harakati zozote za kisiasa,
bila ya kuwa na kibali kutoka kwa viongozi wa serikali ya nchi hiyo.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Tunisia alimetoa taarifa na kusisitiza juu ya
udharura wa kuheshimiwa sheria za nchi hiyo.
Taarifa ya Wizara ya Mambo
ya Nje ya Tunisia imeongeza kuwa, iwapo kundi lolote la Walibya waliopo
nchini humo litakiuka sheria za nchi na kuamua kuendesha shughuli za
kisiasa au kufanya mikutano bila ya kibali cha viongozi wa serikali ya
Tunis, wanachama wa makundi hayo watalazimika kuondoka nchini Tunisia.
Post a Comment