jana likijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki
na kuua waliokuwemo na kujeruhi wengine.
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza,
Valentino Mlowola amethibitisha kuwepo kwa
ajali hiyo.
Amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya
saa 7.40 katika eneo la Mkuyuni, jijini Mwanza
ambapo ilihusisha gari la Benki Kuu (BOT) lenye
usajili namba SU 35296 Toyota Land Cruiser.
Alisema waliokufa ni Beatrice Wanzagi Lumereja
(37) afisa wa BOT na mkazi wa Kiseke na
Dereva Mohamed Mumba (45).
Waliojeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya
rufaa ya Bugando ni pamoja na Sajenti Joel na
PC Jumane waliokuwa wakisindikiza mzigo huo
nyeti pamoja na dereva pikipiki Deus Kalokola
(32).
Alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa
pikipiki namba T 792CTG kuingilia msafara
ghafla.
Hata hivyo Mlowola alisema mzigo huo nyeti
upo salama na kwamba miili ya marehemu
imehifadhiwa katika hospitali ya Bugando
Post a Comment