BREAKING NEWS! YANGA SC,YAMTIMUA RASMI MAXIMO.

Baada ya kuchapwa mabao 2-0 na mahasimu
wao wa soka Simba SC katika mchezo wa ‘
Hisani Nani Mtani Jembe’ siku ya Jumamosi
iliyopita, klabu ya Yanga SC imeamua kufikia
maamuzi magumu ya kumfuta kazi kocha
Marcio Maximo na ni wazi Mholanzi, Hans Van
De Pluijm atachukua nafasi hiyo. Hii ni mara ya
pili kwa Yanga kumfukuza kazi kocha wao mara
baada ya kufungwa na Simba. Ikumbukwe
mwaka uliopita, Mholanzi, Ernie Brandts
aliondoshwa baada ya kufungwa mabao 3-1
katika Mtani Jembe.
Tofauti na ilivyokuwa kwa Brandts ambaye
aliifundisha Yanga kwa mwaka mmoja na
kuisaidia kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania
Bara msimu wa 2012/13, Maximo yeye
amefukuzwa baada ya kuiongoza timu hiyo
katika michezo tisa ndani ya miezi mitatu.
Yanga imepoteza michezo miwili kati ya saba ya
ligi kuu msimu huu, Maximo ambaye alianza
vizuri klabuni hapo kwa ushindi wa mabao 3-0
dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ngao ya
Jamii, alipoteza mchezo wa kwanza tu wa ligi
dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa
Jamhuri, Morogoro.
Yanga imeshinda michezo minne msimu huu,
lakini hadi l,igi inasimama katika raundi ya saba
hakuna mtu alikuwa na shaka kuhusu uwezo
wa Maximo. Kocha huyo wa zamani wa timu ya
Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amechokwa
haraka sana na mashabiki, wapenzi,
wanachama na viongozi wa klabu yake
kutokana na kiwango kidogo cha uchezaji.
Mifumo yake ya ufundishaji imekosa mvuto,
lakini kitendo cha kufungwa kidhaifu na Simba
kimeshindwa kuvumilika.
COUTINHO, JAJA, EMERSON WAMPONZA?
Ndiyo sababu kubwa, ukitoa mbinu zake,
Maximo alikuwa akiwakumbatia zaidi wachezaji
raia wa Brazil, Andrey Coutinho, Geilson Santos
( ambaye aliomba mwenyewe kuachwa baada
ya michezo saba), kwa Emerson Oliveira siwezi
kuzungumzia kwa sababu mchezaji huyo wa
nafasi ya kiungo alicheza katika kiwango cha
kawaida wakati alipoichezea Yanga kwa mara ya
kwanza.
Jaja alifunga mara mbili dhidi ya Azam, ila
alikosa makali katika ligi kuu kiasi cha kufunga
bao moja tu katika michezo saba ya ligi kuu.
Alishindwa kumudu presha ya mashabiki wa
Yanga ambao hawakuwa wakipendezwa na
kiwango chake huku uchezaji wake wa taratibu
ukiwaboa wengi. Maximo aliwanyima nafasi
washambuaji kama Said Bahanunzi, Jerry
Tegete, Saimon Msuva, Hussein Javu na Hamis
Kizza hata pale wachezaji hao wa Kibrazil
waliposhindwa kufanya vizuri.
Kuwang’ang’ania wachezaji hao na kuwanyima
nafasi wale wenye uwezo kumewakera .
Brandts aliondolewa baada ya kufungwa 3-1
licha ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili
zaidi, yeye aliondolewa kwa kuwa alipingana na
uamuzi wa viongozi kuwasajili baadhi ya
wachezaji ambao hakuwataka wakati ule.
Brandts ndiye mwalimu aliyeifanya Yanga
kucheza mchezo mzuri wa kupasiana na ndiye
aliyeimarisha kiwango cha wachezaji kama,
Saimon Msuva, Frank Domayo ( yuko Azam FC
kwa sasa), Juma Abdul, Oscar Joshua na
wengineo lakini kwa Maximo imekuwa ni
tofauti, wachezaji wengi wameshuka viwango
na ameshindwa kuwaimarisha wachezaji ambao
‘ wanasua-sua’. Yanga wamefanya uamuzi
sahihi kwa kumuondoa Maximo na Coutinho.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget