Tume ye uchaguzi inaendelea kutoa matokeo ya uchaguzi wa kihistoria Kenya
Baada ya siku ndefu ya watu kupiga kura nchini Kenya, wengi wana hamu kujua rasmi mshindi wa uchaguzi wa urais. Hata hivyo matokeo ya mwanzo yameanza kutolewa na tume ya uchaguzi na mipaka Kenya, IEBC.
Matokeo hayo yanaonyesha Uhuru Kenyattaanaongoza kwa asilimia hamsini na nne huku mpinzani wake Raila Odinga akiwa na asilimia arobaini na moja.
Taarifa zinazohusiana
Katika ukurasa huu tutaanza kukuletea taarifa kila zinapochipuka kuhusu matokeo ya mwanzo ya wagombea wakuu wa urais kama yanavyoletwa kwetu na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC.
Unaweza kuwasiliana na sisi kutupasha yanayojiri ambako uliko kwenye ukurasa wetu wa BofyaFacebook, Bofyabbcswahili
13:05 Abdulkarim Taraja akiwa Mt Elgon, anasema kwenye Bofyafacebookkuwa anafurahi ambavyo wanaoshindwa wanakubali matokeo ya kura katika eneo hilo
12:59 Blessed Kuriah anasema kwenye ukurasa wa f Bofyaacebook,Bofyabbcswahili, kuwa hali ni tulivu katika eneo bunge la Gatundu Mkoa wa Kati
12:57 Uhuru Kenyatta 2,484,760 Raila Odinga 1,884,152
12:46 Mwandishi wetu Jamuhuri Mwavyombo akiwa mjini Mombasa anasema mji umetulia, maduka mengi yangali yamefungwa watu wakiwa na wasiwasi kuangalia hali itakavyokuwa
12:37 Uhuru Kenyatta 2,459,133 Raila Odinga 1,851, 671
12:24 Idadi ya kura kwa wagombea wakuu wa urais Uhuru Kenyatta 2,429,895 Raila Odinga 1,823,384
12:21 Mwandishi wa BBC Ng'endo Angela ambaye yuko katike eneo bunge la Othaya, Mkoa wa kati, shughuli ya kuhesabu kura inarejelewa upya, baada ya mmoja wa wagombea kutaka hilo lifanyike kufuatia madai ya wizi wa kura. Eneo hilo lina ushindani mkubwa ikizingatiwa lilikuwa eneo bunge la Rais anayestaafu Mwai Kibaki na alikuwa amependekeza mmoja wa wagombea kupigiwa kura na watu wa eneo hilo
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.