Mvua zaleta balaa Arumeru,barabara ya Arusha-Dodoma hatarini kukatika

 picha na google library

Alisema siku hiyo akiwa ndani yeye na familia yake majira ya saa 3.45 walishtukia maji yanaingia ndani mwao na alipotoka na kuchungulia nje alishangaa kuona baadhi ya kuta za nyumba yake zikiwa zimebomoka ,huku uharibifu huo akikadilia kufikia shilingi milioni 50.

''kwakweli vitu vyangu vingi vimeharibika hapa tulipo tupo hatarini ,tunaomba serikali itusaidie ,kwani tupo katika wakati mgumu siwezi kupata usingizi nikihofu kuvamiwa na maji''alisema

Mkazi mwingine,Billy Graham Mathew alisema kuwa maji hayo yamesababisha uharibifu mkubwa baada ya ukuta wa nyumba yake kusombwa na maji huku sehemu kubwa ya nyumba zake zikipatwa na nyufa.

Alisema hali hiyo inatokana na kuziba kwa karavati zilizowekwa na mkandarasi wa kampuni hiyo ,kuwa ndogo na kushindwa kuhimili kishindo cha wingi wa maji hayo yanayotoka kwenye mkondo wa mto kagera.Aliongeza kuwa hali hiyo imesababisha watoto wao kutokwenda shule na baadhi ya huduma muhimu kutopatikana.

Naye meneja wa TANROADS mkoani Arusha,Deosdedit Kakoko,alipoulizwa juu ya athari hizo alisema kuwa ,Tanroads imetuma maombi ya kuomba fedha serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa daraja kubwa kwa kuwa makaravati yaliyopo ni ya muda mrefu yanasitahili kubadilishwa.

Hata hivyo aliongeza kuwa wananchi wanaoishi maeneo hayo wamechangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira kwa kukata miti ovyo na ujenzi wa makazi,hali iliyosababisha mikondo ya maji ya zamani kuvurugika na kumomonyoka kwa udongo  unaoziba kwenye karavati hizo.source princemedia

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget