UTAJIRI wa komediani maarufu
nchini Emmanuel Mgaya ‘Masanja
Mkandamizaji’ ni kufuru! Tena
unatisha na sasa anaonekana
kuwa miongoni mwa wasanii
wanaomiliki fedha na mali nyingi
Bongo, Risasi Mchanganyiko
linakupa zaidi.
Emmanuel Mgaya ‘Masanja
Mkandamizaji’ akiwa mbele ya
usafiri na mjengo wake.
HABARI MEZANI
Awali, habari kuhusu utajiri wa
Masanja ilitua mezani mwa gazeti
hili kama kidokezo, hapo
mwandishi wetu akaingia mzigoni
na kuanza kuchunguza kwa kina
mali anazomiliki msanii huyo na
kugundua kuwa ni kati ya mastaa
mabilionea Bongo.
“Masanja sio yule tena. Ana
mpunga (fedha) mrefu sana.
Hakuna msanii wa maigizo Bongo
anayeweza kumfikia kwa sasa.
Hao wengine ni mbwembwe tu,
lakini pesa imelala kwa Masanja,”
kilipasha chanzo chetu.
Kikaongeza: “Kwanza ana ghorofa
lipo Tabata, hapo ndipo anapoishi.
Pia ana magari kibao ya kifahari,
mashamba ya mpunga na
Kampuni ya OK Security
inayolinda sehemu mbalimbali
zikiwemo taasisi nyeti nchini.
Emmanuel Mgaya ‘Masanja
Mkandamizaji’ akiwa kwenye pozi
na miongoni mwa magari yake.
“Ni msanii gani mwenye kampuni
kubwa kama ya Masanja? Wengi
wanaishia kudai wanatayarisha
filamu ambazo hata matunda yake
hayaonekani.”
Uchunguzi wetu ulibaini ukweli wa
mali za msanii huyo na mambo
mengine mengi yanayoingia kama
vyanzo vya mapato yake.
MAGARI SITA
Ilibainika kuwa, Masanja anamiliki
magari sita, yakiwemo ya kifahari.
Baadhi ya magari hayo ni Toyota
Land Cruiser V8, Nissan Hardboad
na Toyota Verossa.
NYUMBA TATU BONGO
Pia, mkali huyo wa kuvunja
mbavu, anamiliki nyumba tatu za
maana jijini Dar es Salaam, moja
ni ghorofa ipo Tabata, nyingine
Kigamboni na nyingine haifahamiki
eneo rasmi ilipo.
Hata hivyo, imebainika kuwa mbali
na mijengo yake hiyo iliyopo jijini
Dar, nyumbani kwao Mbarali,
Mbeya ana mjengo wa maana.
MASHAMBA KIBAO
Msanii huyo hayupo nyuma
kwenye kilimo, ana mashamba
kadhaa Kigamboni jijini Dar es
Salaam lakini linalotia fora ni lile
lililopo Mbarali lenye ukubwa wa
hekari 50 ambalo analima mpunga.
NI MSANII WAMAIGIZO TAJIRI
ZAIDI?
Kwa utajiri huo, ipo minong’ono
kuwa, nyota huyo anaweza kuwa
kwenye namba za juu za wasanii
wa maigizo wenye mkwanja
mrefu.
Wengine wanaotajwa kwenye
orodha ya waigizaji matajiri Bongo
ni Husna Posh ‘Dotnata’, Mahsein
Awadh ‘Dk. Cheni’ na Amri
Athumani ‘Mzee Majuto’.
MATAJIRI BONGO FLEVA
Katika muziki wa Bongo Fleva,
wasanii wanaoaminika wana utajiri
mkubwa zaidi ni Judith Wambura
‘Lady Jaydee’, Nasibu Abdul
‘Diamond’ na Joseph Haule
‘Profesa Jay’.
Wasanii hao wanamiliki mijengo ya
maana, achilia mbali magari ya
kifahari na miradi kadhaa.
MASWALI KUHUSU MASANJA
Utajiri wa Masanja umeonekana
kuibuka ghafla huku vyanzo vyake
vya kumwingizia kipato
vikijulikana ni sanaa ya uigizaji,
muziki na huduma ya uchungaji.
Je, kwa uigizaji tu katika Kundi la
Orijino Komedi ‘OK’ ndiko
alikopata mkwanja huo na
kuanzisha miradi hiyo mikubwa?
Kama ndiyo, kwa nini memba
wenzake ndani ya kundi hilo
hawana maendeleo makubwa
kama yeye?
Kazi nyingine ya Masanja ni
muziki wa Injili ambapo kwa sasa
albamu yake ya Hakuna Jipya iko
sokoni. Je, albamu hiyo na shoo
anazofanya zinaweza kuwa
chanzo cha utajiri huo?
Lakini pia Masanja ni mchungaji
ambaye anahudumu katika Kanisa
la Evangelist Assemblies of God
Tanzania (EAGT) ‘Mito ya Baraka’
lilicho chini ya Askofu Bruno
Mwakiborwa. Je, mshahara
anaoupata kutokana na huduma
hiyo unaweza kuwa chanzo cha
mapato yake?
Risasi Mchanganyiko halikutaka
kupasua kichwa, juzi lilimsaka
Masanja kwa simu na kumhoji juu
ya mali zake ambapo kwanza
alithibitisha kweli anamiliki mali
hizo na nyingine ambazo
hakupenda kuzitaja.
“Ni kweli nina nyumba tatu hapa
mjini, kampuni ya ulinzi na
mashamba ya mpunga eka 50
nyumbani Mbarali, Mbeya. Kuhusu
magari pia ni kweli kabisa. Mimi ni
mtumishi sitakiwi kusema uongo,”
alisema Masanja.
Post a Comment