WEMA NA PENY KUIPASUA FAMILIA YA DIAMOND KATIKATI soma hapa kujua zaidi........

Katika hali ya kushangaza,
mastaa wawili Bongo,
mwigizaji Wema Isaac Sepetu
na mtangazaji wa
DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’
wanadaiwa kuipasua familia ya
kinara wa Bongo Fleva, Nasib
Abdul ‘Diamond Platnumz’,
Ijumaa Wikienda lina ripoti
kamili.
Kwa mujibu wa chanzo makini
ambacho ni mtu wa karibu na
familia hiyo kuna mgawanyiko
ambao umesababisha mpasuko
unaofanya familia hiyo kuwa
na makundi mawili
yasiyoelewana juu ya uhusiano
wa Diamond na warembo hao.
Kwa sasa Diamond anatoka
kimapenzi na Wema baada ya
kumwagana na Penny lakini
mtangazaji huyo anadaiwa
kuendelea kwenda katika
familia hiyo kwani asilimia
kubwa inaonesha anakubalika
zaidi ya wengine wote.
TEAM PENNY VS TEAM WEMA
Habari zilidai kuwa mpasuko
huo ni mkubwa kwani kundi
moja linalojiita Team Penny
linamkubali zaidi Penny na
lingine ambalo lina watu
wachache Team Wema
linamkubali Wema.
Imefahamika kwamba kundi
linalomkubali Penny na
kumuona ndiye mwanamke
sahihi kuwa na Diamond
japokuwa wameshaachana ni
Mama Diamond mwenyewe,
Sanura Kassim ‘Sandra’, dada
zake Esma Platnumz, Queen
Darleen, Anko na dada wa
hiyari wa Diamond, Halima
Haroun ‘Kimwana’
Ilidaiwa kwamba kundi hilo
limekuwa likitoa ushirikiano
wa karibu mno kwa Penny na
sehemu nyingi wanakuwa wote
ikiwemo kwenye sherehe na
viwanja vya starehe, yaani ni
fulu kujiachia.
Habari hizo zilidadavua kuwa
hata dada wa Diamond, Esma
anaishi nyumba moja na wifi
yake huyo wa zamani.
“Familia ya Diamond
imegawanyika katika makundi
mawili, kundi kubwa
linamkubali sana Penny
japokuwa alishaachana na
Diamond. Ilisemekana kuwa si
familia tu kwani hata madansa
wa Diamond wanampenda sana
Penny kuliko Wema,” kilisema
chanzo.
TEAM WEMA HII HAPA
Uchunguzi wa wanahabari
wetu ulibaini kuwa ndani ya
kundi linalomtaka Wema kuna
watu wachache akiwemo
Diamond mwenyewe, baba
yake, Abdul Jumaa ambaye
kwa upande wake alitamka
wazi: “Wema ndiye mkwe wa
ukweli kabisa.”
Baba huyo alikwenda mbali na
kusema anamkubali Wema kwa
sababu ana nyota kali na ana
roho nzuri hivyo akiendelea
kuwa na mwanaye atakuwa na
mafanikio tofauti na
alivyokuwa na Penny.
Pia ilijulikana kuwa kundi hilo
lina mtu mwingine, ndugu wa
Diamond aitwaye Rommy Jones
ambaye amekuwa akionekana
na Wema mara kwa mara hasa
wakati msanii huyo akiwa
amesafiri.
HALIMA KIMWANA AITWA
KIGEUGEU
Taarifa nyingine zilidai
kwamba katika sakata hilo,
Halima kimwana amekuwa
akiitwa kigeugeu kutokana na
kutokuwa na upande
anaosimamia. “Mara utamuona
na Wema ghafla unamuona
tena na Penny, yule hata
haeleweki. Anajichetua sana,”
kilisema chanzo chetu.
MAMA DIAMOND ANASEMAJE?
“Mimi siwezi kumchagulia
Diamond mwanamke wa kuwa
naye, yeye mwenyewe ataamua
kwa sababu ni mtu mzima kwa
hiyo siwezi kumpangia au
kumchagulia mwanamke wa
kuwa naye,” alisema mama
Diamond bila kukanusha kuwa
na ukaribu zaidi na Penny.
MSIKIE HALIMA KIMWANA
Baada ya kuwatafuta Diamond,
Wema na Penny bila
mafanikio, Ijumaa Wikienda
lilizungumza na Halima
Kimwana ambaye alikuwa na
haya ya kusema:
“Sisi tuko karibu na Penny kwa
sababu anapenda
kujichanganya na sisi hivyo
hata Wema akija kutuchukua
na kutaka twende naye klabu
hatukatai kwa sababu wote ni
mawifi zetu.
“Hatubagui kwani hakuna siku
ambayo Wema alishataka kuwa
na sisi tukamkatalia.”
MASWALI
Hivi karibuni picha za Penny
akiwa na mawifi zake kwenye
shughuli ya kumtoa mtoto wa
ndugu yao zilivuja ambapo
ndani ya sherehe hiyo pia
Diamond alikuwepo akiwa
anacheza dufu lakini Wema
hakuonekana, jambo lililozua
maswali.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget