Katika hali isiyo ya kawaida wakazi wa
manispaa ya singida wameingiwa na
taharuki na kuanza kukimbia ovyo baada
fisi kuonekakana katikati ya mji wa
singida akiwa anakimbia na kuingia katika
maduka ya wafanya biashara.
Wakieeleza kwa hisia tofauti baadhi ya
wakazi huku wengine wakiwa
wamepanda juu ya mapaa ya nyumba
pamoja na watoto wao kwa hofu ya
kuumwa,wamesema kuonekana kwa fisi
mjini katikati ni jambo la ajabu kwani
wanyama kama hao honekana vijiji au
porini,wengine wamesema labda myama
huyo amechelewa kurudi vichakani wakati
alipokuwa amekuja kula mabaki ya
chakula mjini.
Akielezea tukio hilo afisa maliasili mkoa
wa singida Bwana Charles Kidua
amesema pamoja na kwamba wanyama
kama fisi wapo katika manispaa ya
singida na pindi wanapo onekana katika
maeneo ambayo siyo ya kawaida ,Basi
wananchi watoe taarifa kwa mamlaka
husika kwani wanyama kama haho wana
weza kuwa na ugonjwa wa kichaa ,badala
ya kujichukulia hatua mkononi ya
kuwauwa.
Kutokana na umati wa wananchi kuwa
wengi wakati wakimfukuza fisi huyo bila
kujali askari waliokuwa wakituliza fujo
huku wakiwa na silaha,wanachi
walifanikiwa kuwapokonyo askari fisi
baada ya kumtega na kamba huku
wakiimba tunataka fisi wetu na kuamua
kumkimbiza mjini huku wakimpiga umbali
wa kilomita mbili.
Post a Comment