ICC tayari kwa mkutano na Kenyatta

Mahakama ya kimataifa ya ICC, inajianda
kuwa mwenyeji wa mkutano maalum wa siku
mbili kuhusu kesi ya Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta ambaye atakuwa rais wa kwanza
aliye mamlakani kufika mbele ya mahakama
hiyo.
Kenyatta anakabiliwa na tuhuma za uhalifu
dhidi ya binadamu anazodaiwa kutenda baada
ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Mahakama hiyo inasama kuwa Kenyatta
alihusika katika kupanga na kufadhili ghasia za
kikabila baada ya uchaguzi uliozua utata mwaka
2007/08
Zaidi ya wakenya 1,000 waliuawa kwenye gasia
hizo.
Ruto ambaye ni rais kwa muda naye pia
anakabiliwa na kesi katika mahakama hiyo ya
ICC
Mawakili wa Kenyatta wanasema kuwa kesi hiyo
inapaswa kufutiliwa mbali kwa kukosa ushahidi.
Kenyatta ameombwa na mahakama hiyo kufika
mbele yake ili kujadili malalamiko
yaliyowasilishwa na kiongozi wa mashtaka Fatou
Bensouda kwamba serikali ya Kenya imekataa
kuwasilisha ushahidi unaohitajika katika kesi ya
Kenyatta.
Majaji wa mahakama hiyo hata hivyo watathmini
kauli kutoka kwa pande zote mbili.
Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa pia
kutangaza tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi
dhidi ya Kenyatta.
ICC imemtaka Kenyatta kujibu madai ya upande
wa mashitaka kuwa Kenya inakataa kutoa
ushahidi unaotakikana na mahakama hiyo.
Rais Kenyatta akikagua gwaride la heshima
kabla ya kuondoka nchini kuelekea Hague
Mwezi Septemba, mahakama iliahirisha kesi
dhidi ya Kenyatta baada ya upande wa
mashitaka kusema kuwa Kenya imekosa kutoa
ushahidi unaotakikana na mahakama hiyo.
Mashahidi wa upande wa mashitaka
wamejiondoa katika kesi hiyo.
Mamia ya wabunge wa Kenya wanatarajiwa
kuambatana na Kenyatta kama ishara ya
kumuunga mkono.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget