https://www.youtube.com/watch?v=3rmyU5CdmPY#action=share
Mahakama
ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Dar es Salaam imemzuia msanii kutoka
Nigeria, Adedeji Adelek maarufu kama 'Davido' kuperform katika tamasha
la Fiesta linaloandaliwa na Clouds Fm na Prime Promotion, October
18,2014.
Amri hiyo
imetolewa jana (October 17) na hakimu mkazi wa mahakama ya kisutu ,
mheshimiwa D. Kisoka kufuatia maombi ya dharura yaliyowasilishwa
mahakamani hapo na Times Fm Radio na Times Fm Promotion.
Times Fm
Radio na Times Fm Promotion walipeleka maombi ya dharura mahakamani hapo
wakiitaka mahakama kumzuia msanii huyo kuperform katika tamasha hilo
kwa kuwa licha ya BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) kukataa kutoa kibali
cha msanii huyo kwa maelezo kuwa tayari alikuwa ameshachukuliwa kibali
cha kuperform nchini November 1 kwenye tamasha lililoandaliwa na Times
Fm Radio, Clouds Fm na Prime Times Promotion waliendelea na taratibu
zote bila kujali zuio hilo la BASATA.(P.T)
Times Fm
Radio na Times Fm Promotion waliiomba mahakama kuidhinisha madai yao
dhidi ya Clouds Fm, Prime Promotion na mkurugenzi wa kampuni
inayomsimamia Davido, HKN Music.
Madai
hayo ni pamoja na kulipwa fidia ya gharama na usumbufu waliosababishiwa
na walalamikiwa kadiri Mahakama itakavyoona inafaa.
Mahakama
imetoa amri kuwa msanii huyo amezuiwa kufanya onesho hilo October
18,2014 hadi pale ufumbuzi wa kesi hiyo utakapopatikana mhakamani hapo.
Awali,
Davido alisikika katika matangazo ya Times Fm Radio akieleza kuwa
atakuja Tanzania November 1 kwa ajili ya kufanya onesho linaloandaliwa
na kituo hicho cha radio lililopewa jina la 'The Climax',, source mjengwa
Post a Comment