SIMBA NA YANGA HAKUNA MBABE, MANYIKA JR SHUJAA TAIFA...JANGWANI WAKOMA NAYE!

Dida alikuwa wa kwanza kuinusuru timu
yake kufungwa mapema dakika ya sita,
baada ya kudaka shuti la Emmanuel Okwi
aliyepiga ndani ya boksi.
Yanga walijibu shambulizi hilo dakika hiyo
hiyo, baada ya Mbrazil, Genilson Santana
Santos ‘Jaja’ kuiunganishia nje krosi
maridadi ya Oscar Joshua.
Manyika mdogo naye akadaka shuti la
Mbrazil, Andrey Coutinho dakika ya 13 na
kuwakatisha tamaa mashabiki wa Yanga SC
waliodhani yeye ni mwepesi kufunga.
Mshambuliaji Mganda, Okwi tena
aliunganishia nje kwa kichwa krosi nzuri ya
William Lucian ‘Gallas’ akiwa kwenye nafasi
nzuri na kubaki amejishika kichwa
kujilaumu.
Kipindi cha pili, Simba SC ndiyo walioanza
kupeleka mashambulizi na dakika ya 46 tu,
Elias Maguri alipiga juu ya lango baada ya
kupewa pasi nzuri na ‘Gallas’.
Jaja tena aliikosesha Yanga bao dakika ya
73 baada ya kuunganishia juu ya lango
krosi maridadi ya Simon Msuva aliyetokea
benchi kuchukua nafasi ya Haruna
Niyonzima.
Manyika akaokoa tena shuti kali la Jaja
dakika ya 76 na kuzidi kuwakatisha tamaa
Yanga SC na kocha wao, Mbrazil Marcio
Maximo.
Matokeo hayo, yanaifanya Yanga SC itimize
pointi saba baada ya kucheza mechi nne,
ikishinda mbili, kufungwa moja na sare
moja, wakati Simba imeendelea kuokota
pointi moja moja, kwa sare ya nne
mfululizo.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Peter
Manyika, William Lucian ‘Gallas’, Issa
Rashid ‘Baba Ubaya’, Hassan Isihaka,
Joseph Owino, Jonas Mkude/Pierre Kwizera
dk60, Emmanuel Okwi, Said Ndemla/
Shaaban Kisiga dk38, Elias Maguri, Amri
Kiemba/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk81
na Haroun Chanongo.
Yanga SC; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul/
Salum Telela dk70, Oscar Joshua, Kevin
Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu
Twite, Mrisho Ngassa, Hassan Dilunga,
Genilson Santana Santos ‘Jaja’/Hamisi Kiiza
dk82, Haruna Niyonzima na Andrey
Coutinho.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

designed by izack. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget