Tumekuwa tukipata taarifa zinazohusu
matukio ya mauaji ambayo yamekuwa
yakijitokeza mara kwa mara nchini Tanzania,
hali ambayo imeonekana kukithiri katika siku
za usoni huku jeshi la polisi likitoa ahadi ya
kufanya jitihada za kuhakikisha linawatia
nguvuni wahusika wa matukio hayo.
Taarifa iliyonifikia hivi punde kupitia Radio
One Breaking News inahusu kuuawa kwa
mtuhumiwa namba moja wa kesi ya ulipuaji
mabomu jijini Arusha, Yahaya Hassan Omar
kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi
wakati alipojaribu kutoroka akiwa chini ya
ulinzi..
Post a Comment